Skudu Astaafu Kucheza Soka, Kituo Kinachofuata Ukocha
ALIYEKUWA kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mahlatsi Makudubela ‘Skudu’ ametangaza kustaafu rasmi kucheza soka, baada ya safari yake ya miaka 17 ya utumishi uwanjani.
Ameongeza: “Kuanzia shule ya Ubora ya SAFA Transnet mnamo 2004 hadi kucheza kote Afrika Kusini, Jamhuri ya Czech, Georgia, Tanzania, DRC na Angola, kila jezi, kila kipindi cha mazoezi, kila uwanja ulinijenga.
“Shukrani zangu za dhati kwa kila klabu niliyowakilisha
Mamelodi Sundowns, Platinum Stars, Orlando Pirates, Chippa United, Highlands Park, University of Pretoria, Marumo Gallants, Siwelele FC, na kwa ndugu zangu walio nje Karviná FK, FC Gagra, Yanga, AS Vita Club na Wiliete FC.
Skudu alijiunga na klabu ya Yanga Julai 2023 akitokea Marumo Gallants ambapo alitambulishwa kwa aina yake katika sherehe za Wiki ya Mwananchi zilizofanyika Julai 22, 2023.
Siku hiyo, aliingia kwa wimbo wa Amapiano akiongozana na msanii wa Bongo Fleva, Juma Jux, vituko vyake viligeuka burudani kwa mashabiki wa Yanga. Akadumu msimu mmoja wa 2023-2024, akaondoka.
Baada ya kutoa waraka huo wa kustaafu, kuna taarifa za Skudu tayari ameanza kusomea ukocha kama alivyogusia katika aandiko lake la filimbi inayofuata ni ukocha.