news

STARS YAIBUKA NA USHINDI MBELE YA MADAGASCAR

admin September 7, 2021 4:43 pm

 TIMU ya Taifa ya Tanzania inayonolewa na Kocha Mkuu, Kim

Poulsen leo Septemba 7 imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya timu ya taifa ya Madagascar. 

Ni katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia uliochezwa Uwanja wa Mkapa na hakukuwa na mashabiki kutokana na kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.

Mabao ya Stars yalifungwa na Erasto Nyoni kwa mkwaju wa penalti Novatus Dismas na yote yalirudishwa kipindi cha kwanza na ubao ulisoma Tanzania 2-2 Madagascar. 

Kipindi cha pili baada ya mapumziko vijana wa Stars waliweza kujipanga na kusaka ushindi kwa juhudi. 

Pasi ya upendo kutoka kwa nahodha Mbwana Samatta ilikutana na miguu ya Feisal Salum ambaye alipachika bao la ushindi. 

BAADA YA KUIONA YANGA NA FUJO ZAO…TRY AGAIN AGUNA KISHA AFUNGUKA HAYA… USAJILI WA YANGA WAMTISHA SHOMARI…AWAKABIDHI UBINGWA WA LIGI KUU MAPEMA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply