kimataifa

WILLIAN KUMBE HAKUWA NA FURAHA ARSENAL

admin September 8, 2021 1:43 pm


KIUNGO wa zamani wa Arsenal, Willian amesema kuwa hakuwa na furaha hata kidogo zama zile alipokuwa ndani ya kikosi hicho.

Raia huyo wa Brazil alivunja mkataba wake wa mshahara mrefu wa pauni 220,000 kwa wiki akiwa amebakiza mkataba wa mwaka mmoja.

Alisepa hapo na kujiunga na Klabu ya Corinthians ya nchini kwao Brazil na alitumika kwenye michezo 37 tu akiwa na timu hiyo na alitupia bao moja tu.

“Nilikuwa kwenye wakati mgumu sana hakika naweza kusema kuwa sikuwa na furaha nikiwa kwenye timu hiyo.

“Sitaki kuingia ndani sana lakini ieleweke kuwa sikuwa na furaha ndio maana nimeamua kurejea Brazil,” .

Nyota huyo alicheza pia timu ya Chelsea inayoshiriki Ligi Kuu England.

SIMBA YAPIGA HESABU ZA UBINGWA BONGO SIMBA YAFICHA NYOTA WAKE WAWILI WAPYA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply