kimataifa

MTAMBO WA MABAO WASTAAFU

admin September 10, 2021 2:43 am


 MSHAMBULIAJI wa zamani wa Juventus, Mario Mandzukic ametangaza kutundika daluga akiwa na umri wa miaka 35.

Nyota huyo msimu uliopita alikuwa ndani ya Klabu ya AC Milan alikwama kufanya vizuri kutokana na kusumbuliwa na majeraha aliyokuwa nayo mpaka anatangaza kustaafu soka akiwa kikosini hapo.

Ikumbukwe kuwa aliwahi kutumikia timu ya taifa ya Croatia na alicheza jumla ya mechi 88 mpaka anastaafu mwaka 2018.

Pia mshambuliaji huyo amepita katika timu mbalimbali ikiwa ni pamoja na Atletico Madrid,Bayern Munich,Milan,Dinamo Zagreb,Wolsburg,Al-Duhail,NK Zagreb na Marsonia.

Mafanikio makubwa aliyapata akiwa ndani ya Bayern Munich ambapo alitwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2012/13. Mpaka anastaafu soka aliweza kutwaa mataji 23 alitupia mabao 261 katika mechi 261.

MUONEKANO WA UKURASA WA NYUMA GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA COASTAL UNION YAWEKA WAZI HESABU ZAO MSIMU MPYA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply