BIashara United

BIASHARA UNITED KAZI BADO INAENDELEA

admin September 19, 2021 1:43 pm


 WANAJESHI wa Mpakani, Biashara United kwa sasa wanatamba baada ya kumaliza kazi ya dakika 180 kwenye mechi ya awali.

Biashara United iliibuka na ushindi wa bao 1-0 ilipokuwa ugenini dhidi ya DIKHIL na ule wa pili uliochezwa Uwanja wa Azam FC ilishinda mabao 2-0 yaliyofungwa na Ramadhan Chombo wengi wanapenda kumuita Redondo.

Kocha wa Biashara United Patrick Odhiambo amesema kuwa vijana wake wanastahili pongezi kwa kuwa walipambana bila kukata tamaa mwanzo mwisho.

“Wachezaji walikuwa katika hali nzuri na wamepambana kwa ajili ya kupata matokeo chanya na mwisho wa siku wamefanikiwa kupata kile ambacho wanakihitaji.

“Bado kuna kazi kubwa na tunahitaji kupata matokeo hivyo mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kila kitu kitakuwa sawa,” amesema.


SIMBA DAY  NI  KUFURUUUU…WAFUNGA TV KUBWA OKWI AIBUKA UWANJA WA MKAPA KWENYE TAMASHA LA SIMBA DAY

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply