news

STARS KUWAFUATA BENIN LEO

admin October 8, 2021 8:43 am


LEO Oktoba 8 Timu ya Taifa ya Tanzania,Taifa Stars, inatarajia kuondoka leo saa 6 mchana kuelekea Benin kwenye mchezo wa marudiano kufuzu Kombe la Dunia.

Jana, Oktoba 7, Uwanja wa Mkapa, Taifa Stars ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na kupoteza pointi tatu muhimu.

Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Oktoba 10, 2021 nchini Benin ikiwa ni vita ya kusaka pointi tatu muhimu.

Taifa Stars itaondoka na Ndege ya Air Tanzania leo na ina matumaini makubwa ya kuweza kupata ushindi licha ya kuwa mchezo huo utakuwa mgumu.

Kocha Mkuu wa Stars, Kim Poulsen amesema kuwa wanatambua utakuwa mchezo mgumu ila watapambana kusema kwamba walipata nafasi na kushindwa kutumia ambazo walizipata.

“Tulishindwa kutumia nafasi ambazo tumezipata hivyo kwa ajili ya mchezo wetu ujao tutapambana kufanya vizuri na kupata pointi tatu muhimu,” .

Kwenye Kundi J vinara ni Benin wakiwa na pointi 7 huku Tanzania ikiwa nafasi ya tatu na pointi zake ni nne.


KOCHA SIMBA ATAJA SIFA ZA WACHEZAJI ATAKAOWATUMIA WAGHANA KUWAFUATA MASTAA WA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply