news

ZAWAD MAUYA AUNGANA NA MSAFARA WA STARS BENIN

admin October 8, 2021 4:43 pm


 KIUNGO mkabaji wa Yanga, Zawadi Mauya ni miongoni mwa nyota walioibukia nchini Benin akiwa na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Kiungo huyo amejumuishwa kwenye msafara huo ili kuongeza nguvu katika mchezo wa marudio unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 10 nchini Benin.

Sababu ya kuongezwa katika msafara huo ni kuchukua nafasi ya kiungo Mzamiru Yassin wa Simba ambaye ana adhabu ya kadi mbili za njano hivyo ataukosa mchezo ujao.

Kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa jana Oktoba 7 Stars ilipoteza pointi tatu kwa kufungwa bao 1-0 hivyo ina kazi ya kwenda kupindua meza kibabe.

Katika msimamo ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi nne na vinara ni Benin wenye pointi 7 na ile ya pili ipo kwa Dr Congo wenye pointi 5 na nafasi ya nne ipo kwa Madagascar ambao hawajakusanya pointi katika kundi J.

SIMBA WAFUNGUKA SABABU ZA INONGA KUTOJIUNGA NA TIMU YAKE YA TAIFA CONGO MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply