news

BAADA YA KUWACHAPA WABOTSWANA..GOMES ATUPA KIAINA DONGO JANGWANI…

admin October 19, 2021 11:00 am


WAKATI Yanga ikibainisha kwamba inahitaji kusepa na taji la Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2021/22 lililo mikononi mwa Simba, Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes amewachimba mkwara kiaina kuhusu taji hilo.

Juzi Simba ilikuwa na kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao ulichezwa nchini Botswana na Simba kuibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Jwaneng Galaxy.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Gomes alisema kuwa wanatambua ligi ya msimu wa 2021/22 ni ngumu ila uhitaji wao ni kutwaa ubingwa kwa kuwa ipo kwenye hesabu zao.

“Tunajua kwamba ligi ni ngumu na kila timu inapambana kupata ushindi hilo halitupi tabu kwani malengo yetu yapo palepale ni kuona kwamba tunashinda taji la ligi ambalo lipo mikononi mwetu.

“Ukiwatazama wachezaji ambao wapo wote wapo tayari na nguvu ipo kwetu kuweza kufanya vizuri, kila kitu ni mipango na tuna amini kwamba tutafanikiwa,” alisema Gomes.

KISA MECHI DHIDI YA AZAM…NABI APINGA MAAMUZI YA MABOSI WA YANGA…WASALIMU AMRI KUHUSU WANAOM’BEZA KUWA HATAIWEZA NAFASI YA CHAMA…BWALYA AWAJIBU HIVI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply