news

KISA YANGA …MWENYEKITI SIMBA ACHACHAMAA…. AIBUKA NA JAMBO JIPYA HUKO..

admin October 23, 2021 3:00 am


MWENYEKITI wa Simba, Murtaza Mangungu, amewaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaambia wasiogope kasi ya wapinzani wao Yanga huku akiahidi kuubakisha ubingwa wa Ligi Kuu Bara Msimbazi.

Kauli hiyo ameitoa baada ya kuiona Yanga ikiwa kileleni ikiwa na pointi tisa, ikishinda michezo yake mitatu ya ligi katika msimu huu.

Simba yenyewe imecheza michezo miwili kati ya hiyo wametoka suluhu na Biashara United huku ikiwafunga Dodoma Jiji bao 1-0, lililofungwa na Mnyarwanda, Meddie Kagere.

β€œMechi tatu haziwezi kuwapa ubingwa au kututoa kwenye mbio za ubingwa. Ligi ni mbio ndefu na sisi Simba ubingwa wetu uko palepale.

β€œWanasimba waondoe hofu, tupo vizuri kama viongozi katika utendaji, pia benchi la ufundi linaloendelea kufanya maandalizi ya kikosi chao,” alisema Mangungu.

SAMATTA AZIDI KUNG’ARA LIGI YA EUROPA…AFUNGA GOLI MUHIMU DHIDI YA TIMU YAKE YA ZAMANI SIMBA SC YAPIGA HESABU ZA MABILIONI YA CAF…SUTI YA FEI TOTO YAZUA GUMZO….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply