news

WAKATI SIMBA WAKIPITIA MAGUMU..MORRISON ASHINDWA KUJIZUIA..AWATAKA MASHABIKI WA YANGA KUFURAHI….

admin November 3, 2021 6:18 am


MSHAMBULIAJI wa Simba, Bernard Morrison  kupitia ukurasa wake wa Instagram, ameandika kwa wakati huu ambao wanapitia wapinzani wao (Yanga) lazima watakuwa wanafurahia kwa sababu ndivyo mpira ulivyo.

Morisson aliandika ; “Muda mwingine mpira unaweza kutoa maumivu makali na mambo mazuri pia, mechi yetu na Jwaneng Galaxy umetuletea huzuni lakini ni furaha kwa wapinzani wetu, huu ndio uzuri wa mpira wa miguu.”

Mshambuliaji huyo pia amewaomba mashabiki wa klabu hiyo kuendelea kuwa nao pamoja licha ya kuwa kwenye wakati mgumu mpaka sasa.

“Ni mpito tu, tuungane  na mambo yatakuwa sawa, tumekuwa hivi kwasababu yenu hivyo msituache”.

Simba imejikuta ikiwa na wakati mgumu baada ya kutolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika lakini pia hata kwenye Ligi wamekuwa na muenendo mbaya baada ya kuchezesha mechi nne wakishinda miwili na sare mbili.

HII YANGA SIO YA LIGI HII…GOTI LA LWANGA MHHH…SIMBA YAJA NA GIA MPYA… KISA  MATOKEO MABAYA..VIGOGO SIMBA WASHINDWA KUJIZUIA…WAWAVAMIA WACHEZAJI NA KUWAPIGA ‘BITI LA KUFA MTU’..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply