Azam FC

BAADA YA KUWA NNJE KWA MUDA MREFU…PRINCE DUBE ARUDI KUONGEZA NGUVU AZAM FC..UONGOZI WATOA TAMKO….

admin December 3, 2021 4:00 pm


BAADA ya kumaliza kazi ya kusepa na pointi tatu muhimu mbele ya Mtibwa Sugar, matajiri wa Dar hesabu zao kwa sasa ni kuelekea kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar.

Azam FC iliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wao uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar ilikuwa ni Novemba 30, Uwanja wa Azam Complex ambapo mtupiaji alikuwa ni Idris Mbombo kwa pasi ya Bruce Kangwa.

Jana, Desemba 2 kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina kiliaza mazoezi kwa ajili ya kujiwinda na Kagera Sugar.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex na utachezwa saa 1:00 usiku itakuwa ni Desemba 9.

Miongoni mwa nyota ambao wamerejea na kuanza mazoezi ni pamoja na mshambuliaji wao namba moja Prince Dube ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya tumbo na alipofanyiwa matibabu alipaswa kukaa nje kwa muda ili kuweza kurejea kwenye hali yake.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit, amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na hali ya dube ipo sawa

WAKATI YA CHAMA YAKIWA HIVYO..USISHANGAE HAYA YAKITOKEA KWENYE DIRISHA DOGO… KWA BEKI HIII..MHHH..SIJUI…..MORRISON KAIPIGA YANGA CAS..AWAITA UWANJANI…MWANASPOTI LEO..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply