news

KUELEKEA DABI YA KARIAKOO…HITIMANA ASHINDWA KUJIZUIA SIMBA..AFUNGUKA KUHUSU PRESHA YAO…

admin December 6, 2021 5:10 pm

 


WAKATI Simba ikiwa Zambia katika michuano ya Kimataifa, kocha msaidizi wa timu hiyo, Thierry Hitimana raia wa Rwanda amefichua kuwa kuwa bize katika michuano ya kimataifa kusiwafanye wapinzani wao Yanga wakajisahau kuelekea kwenye mchezo wao ujao wa Ligi Kuu Bara kwa kuwa malengo yao ni kushinda mchezo huo.

Hitimana ametoa kauli hiyo ikiwa jana Jumapili Simba ilicheza mchezo wa pili wa hatua ya mtoano kwenye Kombe la Shirikisho Afrika kabla ya kurejea nchini kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga ambao unatarajia kupigwa Desemba 11, mwaka huu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Hitimana alisema kuwa uwepo wao katika michuano ya kimataifa wapinzani wao katika Ligi Kuu Bara wasitumie kama kigezo cha wao kuwa wepesi kwa kushindwa kupata matokeo mazuri kwenye mchezo ujao kwa kuwa wamejipanga vizuri.

“Kitu kikubwa nadhani kila mtu anaelewa ukubwa na presha ya mchezo wa dabi inavyokuwa kwa sababu kila upande umekuwa ukitafuta matokeo ili kuwa katika nafasi nzuri kwenye ushindani wa kuelekea mwisho wa msimu.

“Unajua Simba tunashiriki michuano ya kimataifa lakini haiwezi kuwa sababu ya kushindwa kufanya maandalizi ya mchezo huo popote ambapo tutakuwa hivyo wasifikirie kama tutakuwa wepesi,” alisema Hitimana.

KUELEKEA KARIAKOO DABI…SIMBA KUWACHAJI MASHABIKI WA YANGA TSH 30,000..ISHU NZIMA IKO HIVI… ALICHOSEMA ‘TRY AGAIN’ BAADA YA KUISHUHUDIA SIMBA AKITAABISHWA ZAMBIA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply