News

WAKATI SIMBA WAKISHIKILIA MSIMAMO …GSM AIBUA SHANGWE KWA MKAPA…YANGA KAMA KAWA….

admin December 12, 2021 2:37 pm


WACHEZAJI wa Yanga jana waligawa jezi kwa mashabiki wao waliofika kwenye Uwanja wa Mkapa kushuhudia mechi yao ya Ligi Kuu Bara mzunguko wa nane.

Kitendo hicho kilifanyika baada ya kikosi cha Yanga pamoja na benchi la ufundi kupiga picha ya pamoja kabla mechi hiyo haijaanza.

Jezi ambazo wachezaji wa Yanga waligawa ni hizi mpya ambazo zinatumika msimu huu hali iliyowafanya mashabiki kugombea ili kila mmoja apate.

Utaratibu wa wachezaji wa Yanga kugawa jezi ulianza wakati mchezaji wao Paul Godfrey ‘Boxer’ alipofiwa na baba yake ambapo wachezaji waligawa jezi zenye jina la mchezaji huyo mgongoni.

Wiki sasa kumekuwepo na malalamiko kutoka upande wa Simba kuhusu mkataba wa udhamini wa Ligi Kuu Bara ambao Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wamesaini na GSM na katika mchezo huo ilidaiwa kuwekwa mabango ya mdhamini huyo pamoja na jezi kuwekwa nembo ya mdhamini jambo ambalo walilipinga.

Hata kwenye mkutano na waandishi wa habari kwa ajili ya maandalizi ya mechi hiyo, Simba waligomea wakitaka bango la mdhamini mwenza GSM litolewe, hivyo hata mabango yaliyowekwa uwanjani ilibidi yaondolewe kabla ya mechi hiyo na kubaki ya mdhamini mkuu NBC.

Wakati mabango hayo yakiondolewa siku ya mechi, wachezaji wa Yanga wao walivaa jezi ambazo ziliwekwa nembo ya mdhamini mwenza huyo hali ambayo iliamsha shangwe kwa mashabiki wao wakiimba jina la mdhamini huyo.

BAADA YA KUBANWA MBAVU NA SIMBA…NABI AIBUKA NA KUJITETEA KWA HILI..ATAJA SABABU ZA KUFELI… MECHI YA SIMBA vs YANGA YAZIDI KUTOBOA AFRIKA…MMADAGASCAR AFUNGUKA JINSI INAVYOKUBALIKA KWAO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply