Dr Congo Vs Sierra Leone: Kwenye Vita ya Pointi Tatu
Mashabiki wa soka la Afrika wanatarajia kushuhudia pambano lenye ushindani wakati DR Congo itakapovaana na Sierra Leone katika mchezo wa kufuzu michuano ya AFCON 2027. Ni vita ya kusaka pointi tatu muhimu katika Kundi E, huku DR Congo ikitaka kuendeleza mwanzo wake mzuri na Sierra Leone ikiwa na jukumu la kupambana ili kufufua matumaini yake ya kufuzu.
DR Congo, maarufu kama The Leopards, itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na morali kubwa baada ya kushinda michezo yake miwili ya awali dhidi ya Equatorial Guinea na Zimbabwe. Kikosi hicho kimeonyesha uwezo wa kushindana na sasa kinahitaji kutumia vizuri faida ya kucheza nyumbani ili kuendelea kuimarisha nafasi yake kileleni mwa kundi.
Kwa upande wa Sierra Leone, maarufu kama Leone Stars, huu ni mchezo unaohitaji maandalizi makubwa na umakini wa hali ya juu. Timu hiyo imeanza vibaya kampeni zake baada ya kupoteza michezo miwili ya mwanzo, hivyo safari ya kwenda Kinshasa inakuwa nafasi muhimu ya kutafuta matokeo yatakayorejesha matumaini ya mashabiki wake.
Katika mchezo huu, DR Congo itahitaji kutumia vizuri ubora wa kikosi chake, kasi ya mashambulizi na uwezo wa kutengeneza nafasi za kufunga. Sierra Leone nayo italazimika kuwa imara katika safu ya ulinzi na kutumia kila nafasi itakayojitokeza kuwasumbua wenyeji. Kocha Didier Gomes Da Rosa tayari ametangaza kikosi cha wachezaji 25 kwa ajili ya michezo miwili dhidi ya DR Congo.
Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema. Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Kwa kuangalia msimamo wa Kundi E, DR Congo inaongoza ikiwa na pointi sita baada ya ushindi katika michezo miwili, huku Sierra Leone ikiwa haina pointi baada ya kupoteza mechi zote mbili. Tofauti hiyo inaongeza umuhimu wa pambano hili kwa pande zote mbili, hasa kwa wageni wanaohitaji matokeo chanya ili kurejea kwenye ushindani.
Je, The Leopards wataendeleza ubabe wao na kuwafurahisha mashabiki wa nyumbani, au Leone Stars watafanya maajabu kwa kuvunja rekodi ya wenyeji? Dakika 90 za presha, ufundi na ushindani zinakusubiri katika pambano ambalo kila bao linaweza kubadilisha mwelekeo wa Kundi E. Usikose kufuatilia burudani hii ya soka la Afrika! Ambapo leo meridianbet inaendlea kumwaga maokoto jisajili leo uwemiongoni mwa washindi.