News

SIMBA YAACHA WACHEZAJI TISA….BOCCO, NYONI, WAWA NA KISUBI WATAJWA…

admin December 17, 2021 1:00 pm


Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC itakosa huduma ya wachezaji Tisa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar, utakaopigwa kesho Jumamosi (Desemba 18).

Simba SC wamesafiri kulekea mjini Bukoba mkoani Kagera kusaka alama tatu za mpambano huo, ambao utaunguruma kuanzia saa 10:00 jioni, Uwanja wa Kaitaba.

Meneja wa Simba SC, Patrcik Rweyemamu amesema wachezaji tisa wameachwa kwa sababu mbalimbali ikiwamo kuwa majeruhi, kuugua na matatizo ya kifamilia, lakini kikosi kilichotua jana Alhamis (Desemba 16) Jioni mjini Bukoba kipo tayari kupeleka moto kwa Kagera Sugar na kuendeleza wimbi lao la ushindi.

Wachezaji walioachwa jijini Dar es salaam ni Bernard Morrison, Rally Bwalya, John Bocco, Chris Mugalu, Taddeo Lwanga, Erasto Nyoni, Jeremiah Kisubi, Israel Mwenda na Pascal Wawa.

ALIYETUPIA ‘HAT TRICK’ ATUMA SALAMU YANGA…ATOA ONYO KUHUSU MTEREMKO…. KUELEKEA MECHI YA KESHO…SIMBA WALIA…GONJWA LA AJABU LAVAMIA ROBO TATU YA WACHEZAJI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply