news

ALIYETUPIA ‘HAT TRICK’ ATUMA SALAMU YANGA…ATOA ONYO KUHUSU MTEREMKO….

admin December 17, 2021 1:00 pm


Mshambuliaji wa Maafande wa Jeshi la Magereza ‘Tanzania Prisons’ Jeremiah Juma ameitumia salamu Young Africans, ambayo kwa sasa ipo safari kuelekea mjini Sumbawanga Mkoani Rukwa.

Young Africans itakua mgeni wa Maafande hao keshokutwa Jumapili (Desemba 19) katika Uwanja wa Nelson Mandela.

Jeremiah ambaye mpaka sasa ndiye mchezaji pekee aliyefunga Hat Trick kwenye Mshime Mshike wa Ligi kuu Tanzania Bara msimu huu 2021/22 amesema: “Yanga wasitarajie mteremko, tunawasubiri kwa hamu tuliwaona kwenye mechi zao, lakini niwaombe mashabiki waje kwa wingi waone pira gwaride, tutakomaa na kuweka rekodi Jumapili.”

Tanzania Prisons itakwenda kusaka alama tatu muhimu dhidi ya Young Africans, ikiwa nafasi ya 13 katika Msimamo wa Ligi hiyo kwa kufikisha alama 8, huku wageni wao wakiwa kileleni kwa kumiliki alama 20.

BAADA YA DIRISHA DOGO KUFUNGULIWA….SIMBA WAAMUA KUTOKA NA HILI…JINA LA MOSES PHIRI LACHOMOZA… SIMBA YAACHA WACHEZAJI TISA….BOCCO, NYONI, WAWA NA KISUBI WATAJWA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply