news

KUHUSU USAJILI MPYA SIMBA…UONGOZI WAAMUA KUVUNJA UKIMYA…MANGUNGU AANIKA YOTE HEWANI…

admin December 21, 2021 11:42 am


Mwenyekiti wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, Murtanza Mangungu amesema mipango ya usajili wa Dirisha Dogo inakwenda vizuri na wamejipanga kufanya usajili kwa umakini mkubwa.

Simba inatajwa kuwa kwenye mazungumzo na baadhi ya wachezaji wazawa na wale wakimataifa, ambao wataingizwa kwenye kikosi ili kuongeza nguvu

Mangungu amesema Uongozi unafahamu Mashabiki na Wanachama wanataka kuona timu yao inaimarika kwa kuwa na kikosi imara, ambacho kitafanikisha mpango wa kutetea Ubingwa.

“Tunajua kwamba wengi wanataka kusikia tutafanya nini kwenye wakati huu wa usajili, hatuna presha na jambo lolote,tutafanya usajili wa maana na mzuri.”

“Kikubwa ni kuwa na subira unajua mambo mazuri hayahitaji haraka na kwa na kila kitu kinahitaji mikakati imara,” amesema Mangungu.

Dirisha Dogo la usajili limefunguliwa Desemba 15 na linatarajiwa kufungwa Januari 15, 2022 ambapo kwa sasa timu zimeanza harakati za usajili.

RASMI…YANGA WAMPA ‘TALAKA’ RAMADHANI KABWILI…UONGOZI WAFUNGUKA SABABU HIZI BAADA YA SIMBA KUANZA MCHAKATO WA UWANJA WAO..YANGA NAO WAJIBU MAPIGO… SENZO ‘AWAKA’…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply