News

PAMOJA NA KUTOPOTEZA MECHI YOYOTE…YANGA WAKUSUDIA KUFANYA MAAMUZI HAYA MAGUMU..MWANYETO ATAJWA..

admin December 22, 2021 6:00 pm


UONGOZI wa Yanga umefunguka kuwa kuna uwezekano mkubwa wakaingia sokoni na kusajili beki mmoja wa kati mwenye uwezo mkubwa ili kuwa msaada kwa Dickson Job na Bakari Mwamnyeto ambao ndiyo tegemeo kwa sasa.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga, Thabiti Kandoro alipokuwa anaweka wazi mipango ya timu hiyo kwenye dirisha dogo la usajili ambalo limefunguliwa Desemba 16, mwaka huu na kutarajiwa kufungwa Januari 15, mwakani.

Akizungumza na Spoti Xtra, Kandoro alisema viongozi wametazama kikosi na kupitia ripoti ya mwalimu, wamegundua ili kudumu kwenye ubora walionao sasa ni vema wakasajili beki mmoja wa kati.

“Tunahitaji kuwa na timu iliyotimia kwenye kila idara, ukitazama kwa umakini utagundua Yanga inahitaji kuwa na beki mwingine wa kati, kariba ya kina Mwamnyeto na Job.

“Lengo likiwa ni kuwapunguzia mzigo mzito wale wachezaji, hiyo itasaidia timu kuwa na ubora ule ule ambao sisi tunahitaji kuona kwenye kila mechi,” alisema

BAADA YA KUONA ‘GOZIGOZI’ NYINGI….AZAM FC WAAMUA MAAMUZI MAGUMU SAKATA LA ‘SURE BOY’ KUTUA YANGA… KISA YANGA KUFUNGWA GOLI LA MAPEMA NA PRISONS…NABI ATOKWA POVU…ATAJA UKOMAVU…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply