news

BAADA YA KUZIDI ‘KUKICHAFUA’ NA AL AHALY…MIQUISSONE AINGIA ANGA ZA SAMATTA..

admin December 24, 2021 11:00 am


Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Msumbiji Jose Luis Miquissone ameweka Rekodi ya kuwa sehemu ya wachezaji waliotwaa ubingwa wa CAF Super Cup akiwa na mabingwa wa Afrika Al Ahly.

Miquissone ambaye aliitumikia Simba SC kabla ya kuondoka mwanzoni mwa msimu huu, ameweka Rekodi hiyo usiku wa kuamkia leo, baada ya Al Ahly kuichapa Raja Casablanca kwa changamoto ya mikwaju ya Penati.

Mchezo uliochezwa Uwanja wa Al Rayyan nchini Qatar, ulishuhudia miamba Al Ahly na Raja Casablanca walitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1, ambapo kwa Al Ahly Taher Mohamed alisawazisha bao dakika ya 90 ambalo Yasser Ibrahim alijifunga dakika ya 13.

Kwa upande wa mikwaju ya Penati ambayo iliamua mshindi Al Ahly katika fainali walipachika mikwaju 6 huku Raja Casablanca wakiwa wametupia mikwaju 5.

Kwa mafanikio hayo Luis Miquissone anakuwa miongoni mwa wachezaji waliowahi kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara na kubeba taji la Afrika ngazi ya klabu.

Wengine ambao wamewahi kufanya hivyo ni pamoja na Mbwana Samatta ambaye alikuwa anakipiga Simba SC kisha akaibukia TP Mazembe.

MWAKA TUNAUFUNGA HIVI NA SIMU INAYOKAA NA CHAJI KWA ZAIDI YA  MASAA 72. PAMOJA NA KUKABIDHIWA RUNGU LA USAJILI..NABI AVUNJA UKIMYA..ATUPA KOMBORA KWA UONGOZI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply