news

BAADA YA KIMYA KIREFU…BARBARA AAMUA KUVUNJA UKIMYA SIMBA…ATAJA ISHU YA UWANJA..

admin December 28, 2021 4:00 am


MTENDAJI Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez ameweka wazi kuwa Simba ipo imara na hesabu kubwa ni kutimiza malengo waliyojiwekea kutokana na wachezaji walionao kujituma.

Kwa sasa Simba inapambana kuweza kutetea taji lake ililotwaa msimu uliopita wakivutana kwa kasi na vinara wa ligi ambao ni Yanga wenye pointi 23 huku Simba wakiwa nafasi ya pili na pointi 21.

Barbara amesema kuwa wanazidi kufanya mambo mazuri kwa ajili ya timu na kwa sasa wanapambana kuweza kujenga uwanja.

“Tupo imara kwa namna ambavyo tunafanya hivyo mashabiki wasiwe na mashaka na sisi katika yale ambayo tunafanya, wachezaji wanajituma katika kutimiza majukumu yao.

“Imani yetu ni kwamba tutafanya vizuri kwenye ligi na kwenye Kombe la Shirikisho kwani haya nayo ni mashindano makubwa kimataifa kwa kuwa tupo kuiwakilisha nchi kimataifa, mashabiki wazidi kutuombea,” amesema Barbara.

BAADA YA KUISHUHUDIA SIMBA IKIIUA KMC..PABLO ATIKISA KICHWA ..ASISITIZA MAMBO BADO.. KIPA LA KIMATAIFA LINAKUJA YANGA..NABI AFANYA MAAMUZI MAGUMU..SIMBA YATAMBA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply