Azam FC

KUELEKEA MECHI DHIDI YA SIMBA…AZAM FC WAFANYA MAAMUZI MAGUMU…

admin December 29, 2021 4:00 am

 


OFISA Habari wa Azam FC, Thabiti Zakaria amefunguka na kuelezea maandalizi yao ya kuwamaliza Simba kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Januari Mosi, mwakani huku Simba wakiwa wenyeji wa Azam katika Uwanja wa Mkapa, Dar.

Kwenye michezo yao ya mwisho ya Ligi Azam alimpiga Ruvu Shooting mabao 4-1, huku Simba akimpiga KMC 4-1.

Kwenye msimamo Ligi Kuu Bara, Azam ipo nafasi ya saba kwa alama 15, Simba ikiwa nafasi ya pili kwa alama 21. Kinara akiwa Yanga mwenye alama 23 kabla ya mechi za jana.

Akizungumza na Gazeti la Championi , Zakaria amesema: “Tunaanza mazoezi kesho (leo) maana wachezaji walipata mapumziko baada ya mchezo wetu na Ruvu Shooting.

“Mazoezi yetu tutakuwa tunafanya usiku saa moja maana ndiyo muda wa mechi yetu na Simba.

“Siku zote si rahisi haswa timu kubwa zinapokutana ila sisi kwa upande wetu tumejiandaa na ushindi.

“Wachezaji watakaokosekana kwenye mchezo huo ni Iddy Nado ambaye matatizo yake yanajulikana kuwa yupo nje kwa miezi tisa na Ayoub Lyanga.”

KIMENUKA SIMBA….SAKHO,WAWA, KISUBI NA DUNCAN HATIMA  YAO SHAKANI…MAGORI AKOLEZA MOTO.. HIVI NDIVYO DODOMA JIJI WALIVYOIGA UMAFIA WA SIMBA KUMSAINI WAZIRI JR KUTOKA TUNISIA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply