news

HIVI NDIVYO DODOMA JIJI WALIVYOIGA UMAFIA WA SIMBA KUMSAINI WAZIRI JR KUTOKA TUNISIA…

admin December 29, 2021 6:00 am


SASA ni rasmi mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Waziri Junior ni mali ya Dodoma Jiji baada ya awali kuwaponyoka dakika za mwishoni.

Dodoma iliyokaribia kumnasa mshambuliaji huyo siku ya mwisho ya usajili wa dirisha kubwa, lakini ilishindikana kutokana na uwepo wa dili la kujiunga na timu ya nchini Tunisia.

Licha ya kudumu nchini Tunisia kwa miezi kadhaa, mshambuliaji huyo alikuwa bado hajasaini mkataba na klabu inayoshiriki ligi kuu nchini humo, ikiwapa mwanya Dodoma Jiji kumrudisha kwa kipengele maalum.

Hii ni kusema kwamba, Dodoma Jiji imelazimika kumng’oa nyota huyo mdomoni mwa klabu ya Tunisia (jina kapuni), huku ikiweka uwezekano wa kuuzwa kwenye timu hiyo wakati wowote akihitajika.

Mtendaji mkuu wa timu hiyo, Fourtunatus Johnson, ambaye alilazimika kusafiri hadi nchini Tunisia kwenda kumshawishi mshambuliaji huyo kurudi nchini, ameliambia Mwanaspoti kuwa, ilikuwa ngumu kufanikisha dili hilo, ndio sababu wameweka urahisi wa kumuachia pindi atakapotakiwa na klabu hiyo ya Tunisia.

“Tumefanikiwa kumsajili kweli Waziri Junior baada ya dirisha lililopita dili kutibuka mwishoni, imebidi tumfuate Tunisia ili kutimiza hilo, kama timu tulipomchukulia itamhitaji hatutasita kumuachia wakati wowote” alisema Johnson.

Licha ya afisa habari wa timu hiyo, Moses Mpunga kutoweka wazi lakini kuna uwezekano mkubwa, Waziri Junior akawa mrithi wa David Ulomi, aliyeuzwa nchini Sudan ambapo mshambuliaji huyo atakabidhiwa jezi namba saba iliyokuwa inavaliwa na Ulomi.

KUELEKEA MECHI DHIDI YA SIMBA…AZAM FC WAFANYA MAAMUZI MAGUMU… PAMOJA NA KAZI ZOTE CHAFU ANAZOFANYA..MKUDE ANAFUNGA MWAKA KWA REKODI HII..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply