news

FAMILIA YAHUSIKA MAYELE KUSEPA YANGA… UONGOZI WAVUNJA UKIMYA…WAANIKA ISHU ILIVYO…

admin January 5, 2022 9:00 am


MSHAMBULIAJI tegemeo katika kikosi cha Yanga Mkongomani, Fiston Mayele juzi asubuhi alirejea nyumbani kwao, DR Congo kwa ajili ya kumaliza matatizo ya kifamilia.

Mshambuliaji huyo anaondoka nchini baada ya juzi kutoka kuifungia timu yake bao la kuongoza katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Dodoma Jiji uliochezwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Mkongomani huyo anatarajiwa kuukosa mchezo wa kwanza wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya Taifa Jang’ombe kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Yanga inatarajia kucheza mchezo wake wa kwanza wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya Taifa Jong’ombe leo Januari 5, mwaka huu mchezo utakaopigwa saa 2:15 usiku Uwanja wa Amaan mjini Unguja.

Chanzo cha habari kutoka ndani ya uongozi wa Yanga, alipatwa na msiba wa shemeji yake Ijumaa iliyopita saa chache kabla ya mchezo wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji ambao ulimalizika kwa kushinda mabao 4-0.

Chanzo hicho kilisema kuwa mshambuliaji huyo ruhusa ya kwenda kuhani msiba huo ambaye atarejea nchini Januari 7, mwaka huu na moja kwa moja ataungana na timu Zanzibar.

“Mayele alipanga kuondoka kwenda Congo kuhani msiba wa shemeji yake leo (Jumapili) na ataungana na timu visiwani Zanzibar baadaye,” kilisema chanzo hicho.

Alipotafutwa Makamu Mwenyekiti wa timu hiyo, Frederick Mwakalebela kuzungumzia hilo alisema kuwa

“Ni kweli Mayele hayupo na timu amerejea nyumbani kwao kwa ajili ya kwenda kuhani msiba wa shemeji yake lakini haraka atarejea baada ya kumaliza.”

KUELEKEA MECHI YA LEO MAPINDUZI CUP…UONGOZI SIMBA WATOA KAULI YA KIBABE..USAJILI MPYA WATAJWA… WAKATI SIMBA WAKIPANGA KUSHUSHA ‘FULL’ KIKOSI LEO…KOCHA WA SALLEM VIEW ‘ALIA MAPEMA’..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply