news

BAADA YA WATU KUMLAUMU SANA KWA KUWA NA KIWANGO KIBOVU..BOCCO AIBUKA NA KUWAJIBU..ATAJA BAHATI…

admin January 19, 2022 7:52 am


Nahodha na Mshambulaiji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC John Raphael Bocco amesema suala la kufunga ama kutokufunga katika michezo anayopata nafasi ya kucheza linapangwa na Mwenyezi Mungu.

Bocco ametoa kauli hiyo kufuatia lawama anazoangushiwa na baadhi ya Mashabiki na Wanachama wa Simba SC, kufuatia timu yao kupoteza mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City, huku akikosa nafasi kadhaa.

Mshambuliaji huyo aliyemaliza Ligi Kuu msimu uliopita akiwa kinara wa mabao, amesema anaamini muda ukifika atafunga na kilichotokea jana ni mipango ya Mungu.

“Suala la kufunga ni bahati, muda ukifika na Mungu akipanga nifanye hivyo nitafunga, kikubwa ni kuwa miongoni mwa mastaa wanaocheza Simba SC, nikipata nafasi nitapambana kwa ajili ya kuitetea timu itete mataji.” amesema Bocco

Bocco amekua hapati nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha Simba SC, kufuatia Mshambuliaji Meddie Kagere kupewa nafasi mara kwa mara na kocha Franco Pablo Martin.

PAPE SAKHO ALIAMSHA UPYA SIMBA….DAH..KUMBE NI MORRISON..CHICO ATOA KAULI YA KISHUJAA… BAADA YA KUPOKEA KICHAPO CHA KWANZA..SIMBA ‘WACHUTAMA’…WATUMA UJUMBE HUU KWA MASHABIKI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply