News

KUHUSU HATMA YA LWANGA…AHMED ALLY AANIKA MPANGO WA SIMBA..ADAI WALITAKA KUMTEMA…

admin January 20, 2022 5:00 am


Baada ya mwishoni mwa mwaka jana taarifa kusambaa kuwa Klabu ya Simba ina mpango wa kuvunja Mkataba wake na Kiungo Mganda Taddeo Lwanga baada ya kupata majeraha na taarifa zilidai atakaa nje kwa muda mrefu.

Sasa ukweli ni kwamba kiungo huyo mkata umeme, anarejea Uwanjani mwishoni mwa Januari hii kwa mujibu wa Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Wekundu wa Msimbazi, Ahmed Ally.

“Thadeo Lwanga ilikuwa tusitishe mkataba wake mwezi huu kutokana na jeraha lake kuchelewa kupona na tulikuwa tayari kutafuta mbadala wake ila daktari ametuhakikishia atakuwa amepona kufikia mwisho wa mwezi huu (January)” amesema Ahmed Ally.

Urejeo wa Lwanga ni faida kubwa kwa Simba ambayo ratiba yake ni ngumu kwa miezi miwili ya hivi karibuni, wakiwa na mfululizo wa mechi nyingi katika muda mfupi.

Hivyo urejeo wa Kiungo huyo utatoa nafasi kwa Mwalimu Pablo kuwa na machaguo mengi uwanjani, na kufanya mabadiliko ya wachezaji hivyo kuwaepusha nyota wake na uchovu.

SIKU CHACHE BAADA YA KUKARIBISHWA YANGA…MBRAZILI WA MAKIPA ATOA ‘KOMENTI’ HII KWA MSHERY… A-Z JINSI YANGA WALIVYOICHAKATA MBUNI JANA…MUKOKO AMDUWAZA NABI…BRYSON NUSURA AFE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply