news

FT: KAGERA 1-0 SIMBA….KIIZA AWAMWAGIA UPUPU SIMBA…AKIMBIA UWANJANI…ONYANGO, INONGA WAPOTEANA…

admin January 26, 2022 3:48 pm


KLABU ya Simba imeshindwa kutamba katika uwanja wa Kaitaba baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0, kutoka kwa wenyeji wao Kagera Sugar.

Bao hilo la Kagera limewekwa kimiani na mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, Hamis Kizza ‘Diego’ baada ya mabeki wa Simba  wakiongozwa na Henock Inonga na Joash Onyango kudhani kuwa nyota huyo ameotea.

Nyota huyo ambaye aliondoka Simba mwaka 2016, aliipatia timu yake bao hilo dakika ya 71, huku likiwa ni la kwanza tangu asjiliwe katika dirisha dogo la usajili akitokea timu ya Proline FC inayoshiriki ligi daraja la kwanza ya nchini kwao Uganda.

Licha ya Kiiza kuipatia timu yake bao hilo ila alionyeshwa kadi nyekundu kufuatia kukusanya kadi mbili za njao kutokana na kucheza madhambi kwa wachezaji wa Simba kwa nyakati mbalimbali.

Kipigo hicho kwa Simba kinakuwa ni cha pili msimu huu baada ya awali kufungwa bao 1-0 na Mbeya City Januari 17, mchezo uliochezwa katika uwanja wa Sokoine.

Kwa upande wa ‘Wanankurukumbi’ huo unakuwa ushindi wao wa pili mfululizo baada ya mchezo uliopita kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, dhidi ya Dodoma Jiji Januari 21.

Matokeo hayo yanaifanya Simba kusalia nafasi ya pili na pointi 25, hivyo kuwa nyuma ya pointi 10, kutoka kwa wapinzani wao Yanga wenye 35, huku kwa Kagera Sugar wakisogea mpaka nafasi ya tisa baada hapo awali kuwa ya 11, wakijikusanyia pointi 16.

WAKATI MKIZANI SIMBA IMEKWISHA …PABLO AMEWATAZAMAA WEE..KISHA KAIBUKA NA NENO HILI MOJA TU… WAKATI YANGA ‘WAKIENJOY’ SOKA LA PASI SAMBUSA…EL MERRIKH YA SUDAN WAMTAKA TENA NABI..ISHU IKO HIVI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply