Yusuph Kagoma Simba SC
Simba SC

Yusuph Kagoma Arejea Simba SC: Ahmed Ally Athibitisha Habari Njema Mazoezini

Vardo August 31, 2026 11:13 am

Mashabiki wa Simba SC wamepokea habari njema kufuatia kurejea rasmi kwa kiungo wao mahiri, Yusuph Kagoma, ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa muda akiuguza jeraha.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amethibitisha kuwa nyota huyo amerejea mazoezini na yupo kwenye hali nzuri ya kusaidia timu hiyo katika michezo inayofuata. Kagoma ameshajiunga na wenzake kambini huku maandalizi ya mechi zijazo yakiendelea.

“Tunatangaza rasmi Kagoma anarejea tena kuja kujumuika na Wanasimba wenzake katika kupigania heshima ya Simba Sports Club,” alisema Ahmed Ally wakati akizungumzia hali ya kikosi.

Kurejea kwa Kagoma kunatoa nafuu kubwa kwa benchi la ufundi la Simba, ambalo limekuwa likikabiliwa na changamoto ya majeraha pamoja na adhabu za kadi kwa baadhi ya wachezaji muhimms.

Hali ya Majeruhi na Wachezaji Wasiokuwepo:

  • Shomari Kapombe: Beki na nahodha huyu bado yupo nje ya uwanja akiendelea kuguza jeraha la bega alilopata nchini Rwanda.

  • Nickson Kibabage: Beki wa kushoto anaendelea na mpango wa matibabu chini ya uangalizi wa madaktari kabla ya kupewa ruhusa ya kurejea uwanjani.

  • Ibrahim Juma & Antony Mligo: Wachezaji hawa watakosa mchezo unaofuata pekee wanapokamilisha adhabu zao za kadi, kabla ya kurejea kikosini kwenye mechi inayofuata.

Benchi la ufundi linaendelea kusubiri kupona kwa akina Kapombe na Kibabage ili kuwa na kikosi kamili na imara zaidi kwenye michezo ya mbele.

SEO Title: Vita ya Makocha NBC Premier League: Makocha Wazawa Kukiwasha Dhidi ya Wageni Leo Ally Mayai Amchambua Ibrahim Doumbia Simba SC: Aainisha Udhaifu na Njia ya Kufanikiwa