News

BAADA YA KUWA MAJERUHI KWA MUDA MREFU…UONGOZI YANGA WAJA NA HILI KUHUSU YACOUBA…

admin February 15, 2022 5:00 am

 


KIUNGO wa Yanga, Yacouba Songne, yupo kwenye hatua za mwisho za kuimarika afya yake kabla ya kuungana na timu na kufanya mazoezi ya pamoja kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC).

Yacouba kwa sasa yupo kwenye program maalumu chini ya kocha wa viungo ambayo inamrejesha taratibu kwenye hali yake ya kawaida na huenda wiki ijayo ataungana na wenzake katika viwanja vya mazoezi.

Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga, Thabity Kandoro, alisema kuwa alikuwepo kwenye uwanja wa mazoezi juzi na aliona namna ambavyo Yacouba anatia matumaini na anaonyesha amebakiza siku chache ili aweze kurejea uwanjani.

“Yacouba huenda wiki ijayo akaanza mazoezi ya uwanjani, kwa maana nilivyomuona juzi anaonekana hana muda mrefu. Kwa sasa yupo chini ya program ya kocha wa viungo na huenda wiki ijayo akaungana na wenzake,” alisema.

Yacouba yupo nje ya uwanja kwa muda sasa akiuguza majeraha ya goti ambayo aliyapata kwenye mechi ya ligi na kulazimika kufanyiwa upasuaji.

WAKATI WAMOROCCO WAKIENDELEA KUMKAUSHIA…MSUVA AVUNJA UKIMYA…ATAJA MSIMAMO WAKE… BAADA YA KUONA VIWANGO VYA MAKIPA YANGA…MBRAZILI AGUNA KISHA AKATOA HILI..ADAI ITAKUWA NGUMU…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply