News

WAKATI WAMOROCCO WAKIENDELEA KUMKAUSHIA…MSUVA AVUNJA UKIMYA…ATAJA MSIMAMO WAKE…

admin February 15, 2022 5:00 am


KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva, amesema kuwa Watanzania wanatakiwa kuwa watulivu na muda ukifika ndiyo ataweka wazi kila kitu kuhusu anachopitia kwa sasa kwenye soka.

Msuva alifunguka kuwa akili yake kwa sasa anaielekeza kwenye kufanya mazoezi zaidi ili kuendelea kuwa fiti na ndiyo maana amekuwa mgumu kuzungumza na vyombo vya habari kwa kuwa muda wa kufanya hivyo bado haujafika.

Akizungumza na gazeti la  Championi , Msuva alisema yeye ndiye anajua kila kitu kuhusu wapi atacheza msimu ujao na nini kinaendelea juu ya masuala yake ya kimkataba na klabu ya Wydad Casablanca na wakati wa kuweka wazi ukifika atasema na watu wanapaswa kuwa watulivu.

“Watanzania watulie tu kwa sasa, mimi nitasema muda ukifika nini kinaendelea kwangu, kwa sasa akili yangu naelekeza zaidi kwenye kufanya mazoezi ili kuendelea kuwa fiti zaidi,” alisema Msuva.

Msuva yupo nchini takribani miezi miwili sasa, ikidaiwa ameondoka Wydad Casablanca kwa sasa, anahitaji kulipwa maslahi yake ya kimkataba ikiwemo fedha za usajili, huku taarifa zikiibuka kuwa TP Mazembe wapo wanawinda saini yake pia.

INONGA ARUDISHA MKWANJA WA YANGA…AMKIMBIA MAYELE AIRPORT…SIMBA WAPEWA MCHONGO CAF… BAADA YA KUWA MAJERUHI KWA MUDA MREFU…UONGOZI YANGA WAJA NA HILI KUHUSU YACOUBA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply