News

BEKI WA SIMBA ASHINDWA KUJIZUIA KUHUSU MAYELE…AFUNGUKA JINSI ALIVYOMTESA PAMOJA NA ‘KUMCHEZEA KAZI CHAFU’

admin February 26, 2022 11:00 am


BEKI wa kati wa Simba anayekipiga kwa mkopo Mtibwa Sugar, Ibrahim Ame, amesema mshambuliaji wa Yanga, Mkongomani, Fiston Mayele ameshindikana huku akisisitiza amemkosesha usingizi.

Kauli ya beki huyo imekuja baada ya mchezo wa Ligi Kuu Bara kumalizika kwa Yanga kuwafunga Mtibwa mabao 2-0 juzi Jumatano kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.

Ame alisajiliwa na Simba msimu uliopita akitokea Coastal Union ya Tanga ambaye msimu huu alitolewa kwa mkopo Mtibwa pamoja na Said Ndemla na Jeremiah Kisubi.

 Ame alisema kuwa kabla ya mchezo huo, alipewa jukumu la kumkaba Mayele kwa lengo la kutofunga, lakini imeshindikana baada ya kumruhusu mshambuliaji huyo kufunga bao. Ame alisema kuwa bao hilo alilofunga Mayele, limemfanya akose furaha na amani huku akishindwa kupata usingizi.

Ame ambaye alishindwa kuendelea na mchezo baada ya bao hilo kutokana na maumivu, alionekana akiwa chini nje ya uwanja akisononeka. “Mayele ni mshambuliaji hatari na wa kuchungwa akiwa uwanjani kutokana na kiwango chake bora.

“Nakumbuka kabla ya mchezo wetu huo, nilipewa jukumu la kutembea na Mayele kila sehemu kwa lengo la kutofunga, lakini ikashindikana na kupata upenyo akafunga.

“Kiukweli nilifanya jitihada nyingi za kutosha za kuhakikisha Mayele hafungi lakini nimeshindwa, alitumia nafasi moja aliyoipata kufunga, kiukweli siku yangu imeharibika baada ya bao hilo, sitaweza kupata usingizi,” alisema Ame.

MAKAME AANIKA MAISHA YA SIRI YA ‘FEI TOTO’…ADAI ANAPENDA KUOMBAOMBA KILA KITU…WALIKUWA WANAMCHEKA… FISTON NA KISINDA WAUNGANA KUITISHIA ‘NYAU’ SIMBA..WATOA MKWARA MZITO UTAFIKIRI WAO NI MESSI NA RONALDO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply