CAF

FISTON NA KISINDA WAUNGANA KUITISHIA ‘NYAU’ SIMBA..WATOA MKWARA MZITO UTAFIKIRI WAO NI MESSI NA RONALDO…

admin February 26, 2022 11:00 am


KUELEKEA mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Simba, wachezaji wa zamani wa Yanga, Tuisila Kisinda na Fiston Abdoul Razak, wametoa mbinu jinsi ya kuwamaliza wapinzani wao hao kwa kuwa wanawajua kutokana na kuwahi kukabiliana nao walipokuwa Bongo.

Kisinda na Fiston kwa sasa wameungana tena wakiichezea Berkane ya Morocco. Mchezo wao huo utachezwa keshokutwa Jumapili, Casablanca, Morocco, huku Simba wakiwa ndiyo vinara wa kundi lao la D kwa alama 4.

Wawili hawa waliondoka Yanga msimu uliopita. Kisinda aliuzwa na Fiston alimaliza mkataba. “Tunawajua Simba na tumejipanga kuweza kuzibeba alama tatu muhimu kutoka kwao maana ni timu ninayoijua sana,” alisema Kisinda.

“Maandalizi yetu yapo vizuri tunajua kuwa Simba huwa ni bora sana kwenye michuano ya kimataifa na sisi ni bora zaidi yao na tutawapiga, maana tunawajua,” alisema Fiston.

BEKI WA SIMBA ASHINDWA KUJIZUIA KUHUSU MAYELE…AFUNGUKA JINSI ALIVYOMTESA PAMOJA NA ‘KUMCHEZEA KAZI CHAFU’ PAMOJA REKODI NZURI YA SIMBA DHIDI YA IBENGE….PABLO AINGIA UBARIDI…AFUNGUKA WASIWASI WAKE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply