Yanga SC vs Gaborone United
Yanga SC

Komara Aipa Yanga SC Onyo Zito Ikielekea Botswana Kukipiga na Gaborone United

Vardo September 2, 2026 9:43 am

USHINDI walioupata katika mchezo uliopita unaweza kuwa umeongeza morali ndani ya kikosi cha Yanga SC, lakini beki kisiki Farouk Komara amesisitiza kuwa hakuna nafasi ya kubweteka, akitaka timu hiyo kuelekeza nguvu zote kwenye changamoto mpya ya kimataifa.

Yanga SC sasa inajiandaa kuvaana na Gaborone United ya Botswana katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa Jumamosi, Septemba 5, 2026. Pambano hilo litakuwa ndio mwanzo rasmi wa safari yao katika michuano hiyo mikubwa zaidi barani Afrika kwa msimu huu.

Kikosi cha Yanga tayari kimeondoka leo kuelekea Botswana tayari kuanza kampeni yao ya kusaka alama tatu muhimu ugenini.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, Komara amesema matokeo mazuri waliyoyapata nyuma hayapaswi kuwafanya wachezaji kushusha kiwango, badala yake yawe chachu ya kuongeza juhudi na kujiandaa zaidi kwa pambano hilo lenye umuhimu mkubwa.

“Tunapaswa kusahau haraka mchezo uliopita na kuanza kuangalia mbele. Kila mchezo una changamoto zake na huu wa kimataifa unahitaji maandalizi ya aina yake,” amesema Komara.

Beki huyo amesisitiza kuwa mchezo dhidi ya Gaborone United utahitaji umakini wa hali ya juu kutoka kwa kila mchezaji, huku nidhamu ya mchezo ikiwa silaha kuu itakayowabeba kupata matokeo mazuri ugenini.

Kwa mujibu wa Komara, Yanga inapaswa kuingia uwanjani ikiwa na dhamira ileile ya kupambana hadi dakika ya mwisho. Ameongeza kuwa kila mchezaji anatakiwa kutimiza wajibu wake ili kuhakikisha timu inabaki imara wakati wote wa mchezo.

Vita ya Clean Sheets: Kassali na Diarra Watengeneza Rekodi Ligi Kuu Mngqithi Afichua Mbinu Mpya Yanga vs Gaborone United: Aziz Ki Areyewa Mpango Maalum!