news

KUELEKEA MECHI DHIDI YA SIMBA…IBENGE AWEWESEKA NA UWANJA WA MKAPA…AKIRI MAMBO MAGUMU …

admin March 9, 2022 10:43 am


KOCHA wa RS Berkane ya Morocco, Florent Ibengé amesema kuwa mpira wa Simba wanapokuwa katika uwanja wao wa nyumbani ni kikwazo kuelekea katika mchezo wao wa marudiano wa michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Simba wanatarajiwa kuwakaribisha RS Berkae katika mchezo wa marudiano unaotarajiwa kufanyika Machi 13, katika Uwanja wa Mkapa. Simba wanaingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa mabao 2-0 ugenini.

Kocha Ibenge aliweka wazi kuwa anazikumbuka mechi ambazo amekutana na Simba katika Uwanja Mkapa huku akiwa na kumbukumbu ya kutokupata hata sare jambo ambalo linampa wakati mgumu kuelekea katika mchezo huo.

“Hakuna ambacho hakipo wazi, nimepoteza michezo mingi, sina kumbukumbu ya kushinda dhidi ya Simba katika uwanja wao, ni rekodi mbaya kwangu lakini sitaki kuona ikijirudia safari hii kwa kuwa kuna mengi yamebadilika katika mpira sio historia mara zote.

“Malengo yetu ni kushinda michezo mingi zaidi ili tuweze kusonga mbele katika michuano hii, katika kundi letu utofauti unatakiwa kuuonyesha katika kupata matokeo ya ugenini, tunatakiwa kufanya hivyo,” alisema kocha huyo.

RASMI…”MCHAWI MWEUSI’ KUTOKA AFRIKA KUSINI PITSO MOSIMANE APATA ‘SHAVU’ JIPYA AL AHLY…WAARABU WANUNA.. BAADA YA CAF KUIPA SIMBA SC MASHABIKI…AHMED ALLY KAFIKIRIA WEEE..KISHA AKAIBUKA NA KAULI HII YA KIBABE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply