news

RASMI…”MCHAWI MWEUSI’ KUTOKA AFRIKA KUSINI PITSO MOSIMANE APATA ‘SHAVU’ JIPYA AL AHLY…WAARABU WANUNA..

admin March 9, 2022 7:04 am


Kocha Mkuu wa Klabu ya Al Ahly ya Misri, Pitso Mosimane (57) raia wa Afrika Kusini ameongeza mkataba mpya wa miaka miwili wa kuendelea kuitumikia timu hiyo hadi msimu wa mwaka 2023/24.

Mosimane alitangazwa rasmi kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo Oktoba mwaka 2020 akitokea ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Taarifa hii imethibitishwa na Al Ahly wenyewe ambao kupitia kurasa zao za kijamii na tovuti wametangaza juu ya mkataba huo mpya ambapo pia wasaidizi wa kocha huyo nao wameongeza mkataba wa miaka miwili.

Awali ilikuwa ikiaminika kocha huyo atafukuzwa au kuondoka klabuni hapo baada ya mkataba wake kuwa unaelekea ukingoni, wakongwe kadhaa wa Al Ahly waliowahi kucheza kikosini hapo na wachambuzi wa Misri walikuwa wakimshutumu kuwa hana uwezo wa kuifundisha timu hiyo.

KUHUSU UBINGWA MSIMU HUU..YANGA WAIJIBU SIMBA KIBABE…BUMBULI AWEKA HADHARANI ISHU ILIVYO… KUELEKEA MECHI DHIDI YA SIMBA…IBENGE AWEWESEKA NA UWANJA WA MKAPA…AKIRI MAMBO MAGUMU …

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply