Habari za michezo

KISA TABIA ZA MAYELE..SENZO ASHINDWA KUJIZUIA…ATOA ONYO KALI..SIMBA WATAJWA…

admin March 22, 2022 12:14 pm


KASI ya ufungaji mabao aliyonayo mshambuliaji Mkongomani wa Yanga, Fiston Mayele kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu imemuibua Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Senzo Mbatha ambaye ameweka wazi kuwa wapinzani wao katika michezo ijayo wakiwemo Simba wajipange kwani Mayele ataendelea kutetema.

Mayele juzi Jumamosi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC alipiga shuti lililosababisha KMC wakajifunga katika kipigo cha mabao 2-0. Bado ana mabao 10 kwenye ligi akiwa kileleni kwenye chati ya wafungaji, sawa na Reliants Lusajo wa Namungo.

Ushindi huo umeifanya Yanga kufikisha pointi 48 zinazowafanya waendelee kuongoza msimamo wa Ligi Kuu mara baada ya kucheza michezo 18, ambapo ratiba ya michezo yao miwili ijayo ni dhidi ya Azam Aprili 6 na Simba Aprili 30, 2022.

Senzo alisema: “Kwangu sishangazwi na uwezo wa Mayele, huyu ni miongoni mwa wachezaji bora zaidi tuliowasajili msimu huu, ana nidhamu kubwa na licha ya uwezo anaouonyesha bado anaonyesha jitihada kubwa mazoezini.

“Nadhani wapinzani wetu katika michezo ijayo wanapaswa wajipange, kwani ninaamini Mayele atawafunga sana katika michezo yetu ijayo.”

UKWELI NI KWAMBA..MORRIOSN NI MCHEZAJI FULANI WA MCHONGO MCHINGO HIVI…BASI TU YANI… KUHUSU ISHU YA SIMBA KUWA BINGWA TENA MSIMU HUU…WAWA KAGUNA KWANZA..KISHA AKASEMA HAYA..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply