Habari za michezo

RASMI…WASAUZI WAGOMA KUMRUHUSU MORRISON KUINGIA KWAO…BARBARA AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA…

admin April 12, 2022 10:55 am


KIUNGO mshambuliaji wa klabu ya Simba raia wa Ghana Bernard Morrison sasa ni rasmi kuwa hawezi kwenda nchini Afrika Kusini kutokana na kufungiwa kuingia ndani ya nchi hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa klabu hiyo Barbara Gonzalez amethibitisha hilo rasmi kuwa jitihada zilizofanyika za kumuombea kibali cha kuingia nchini Afrka Kusini zimegonga mwamba.

Barbara alisema: “Tuliwasiliana na watu wa Mamlaka ya Uhamiaji Afrika Kusini kuomba kupata ruhusa ya kuingia na Morrison, walitueleza sharia zao mtu akivu nja hawezi kupata tena nafasi ya kuingia,”

“Wametuambia kutokana na kosa lake Mamlaka haipo tayari kumruhusu kutokana na sharia zilivyo, hivyo ni rasmi sasa Morrison hataenda Afrika kusini. Tutamjulisha kocha ili afahamu hilo na kuona jinsi ya kujipanga kwa mechi ya ugenini bila ya Morrison.”

Klabu ya Simba inatarajiwa kucheza na Orlando Pirates ya Afrika Kusini katika hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mnamo Aprili 17 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kama.

Mchezo wa marudiano unatarajiwa kupigwa katika Uwanja wa Orlando uliopo jijini Johannesburg Afrika Kusini mnamo Aprili 24 mwaka huu.

SIMBA WAZINDUA KAMPENI YA KUWAMALIZA WASAUZI KWA MKAPA…MZEE DALALI AMWAGA ‘ASALI’…. KUELEKEA MECHI YA CAF…WASAUZI WAIFANYIA SIMBA UMAFIA HAPAHAPA TZ…MASHUSHU WAMWAGWA KILA KONA..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply