Habari za michezo

BAYERN KUMPA MKATABA ‘KUFURU’ LEWANDOWSKI ..BARCELONA WACHUNGULIA ..KISHA WARUDISHA SHINGO NDANI..

admin April 15, 2022 2:52 am

 


Klabu ya Bayern Munich imeaandaa ofa ya mkataba wa miaka 2 wanaotaka kumuongeza mshambuliaji wa kabu hiyo Robert Lewandowski. Mshambuliaji huyo amaekuwa akihusishwa kujiunga na FC Barcelona mwishoni mwa msimu huu.

Mkataba wa Lewandoski raia wa Poland mwenye umri wa miaka 33 na Bayern Munich unamalizika Juni mwaka 2023. Na amekuwa akitajwa huwenda akajiunga na FC Barcelona kwa ada ya uhamisho ya Euro million 60 ambayo ni zaidi ya billion 150 kwa pesa za kitanzania (150,533,605,064.23).

Chanzo kimoja kutoka Ujerumani kimeripoti kuwa FC Barcelona waliuliza taarifa zinazohusu mkataba wa Lewandoski na hatma yake lakini hakuna Offa yoyote ya usajili ambayo klabu hiyo kutoka Hispania imepeleka kutaka kumsaji.

Huu ni msimu wa 8 kwa Lewandoski akiwa na kikosi cha The Bavrians na tayari amaichezea jumla ya michezo 370 katika michuano yote na kafunga mabao 341. Msimu huu unaoendela wa 2021-22 tayari amefunga mabao 47 kwenye michezo 41 kwenye mashindano yote.

BAADA YA PABLO KUAMUA KUMWEKA KANDO  KIKOSINI……DILUNGA AAMUA KUMTIMKIA AFRIKA KUSINI… USAJILI WA ONYANGO YANGA WAZIDI KUPINGWA…DISMAS TEN AIBUKA NA KUFUNGUKA HAYA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply