Habari za michezo

RASMI…SIMBA WAANIKA KOSA ALILOFANYA MORRISON HADI AKAZUIWA KUINGIA AFRIKA KUSINI…

admin April 15, 2022 6:00 pm


KLABU ya Simba imefafanua sababu za mchezaji wake, Bernard Morrison kuzuiliwa kuingia nchini Afrika Kusini baada ya kufanya makosa nchini humo.

“Morrison ana shida zake binafsi na mamlaka ya uhamiaji ya Afrika Kusini na kosa alilofanya aliover stay…yaani muda wake wa kuishi Afrika Kusini uliisha, amefungiwa Kama sikosei ni miaka 5 kuingia Afrika Kusini kutokana na hiyo kesi yake.

“Kama Simba tulijaribu kuingilia kati kuhakikisha ni Kwa namna gani suala hili linamalizika lakini kumekuwa na ugumu kidogo kwa hiyo sisi Kama Simba tumeamua ku-give up na kwa mantiki hiyo Bernard hatakuwa sehemu ya kikosi pindi tutakapoelekea Afrika Kusini kwenye mechi ya marudiano,” Meneja Habari na Mawasiliano wa @simbasctanzania @ahmedally_

Morrison ambaye aliwahi kuichezea Orlando Pirates kabla ya kujiunga na AS Vita ya Congo DR kisha Yanga na baadaye Simba hatokuwa sehemu ya kikosi hicho kitakachokwenda Afrika Kusini wakati wa duru ya pili ya marejereano ya mechi ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na kati ya Simba na Orlando.

FEI TOTO – NAUMIA..NATAMANI KUCHEZA…SIJUI NITAANZA LINI… PANDA SHUKA YA BOCCO NA KAGERE YAMUIBUA METACHA…AFUNGUKA HALI JINSI ILIVYO WAKIKUTANA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply