Fahyma na Rayvanny
Burudani

Fahyma na Rayvanny: Rekodi ya Video 7 za Mapenzi na Maajabu Yake Bongofleva

Vardo August 16, 2026 11:31 am

STAA wa Bongofleva na Mkurugenzi wa Next Level Music (NLM), Rayvanny, pamoja na mpenzi wake wa muda mrefu ambaye ni mwanamitindo mashuhuri, Fahyma, wanaendelea kuthibisha kuwa uhusiano wao si wa kimapenzi tu bali pia ni wa kibiashara na sanaa.

Wawili hawa ambao wamekuwa pamoja kwa zaidi ya miaka 10 na kubarikiwa mtoto mmoja (Jaydan), hivi karibuni wamewasha tena moto baada ya Fahyma kuonekana kwenye video mpya ya Rayvanny ya wimbo “Touch” (2026), uliotayarishwa na producer S2kizzy kutokea studio za Pluto Republic.

Rekodi ya Kipekee ya Fahyma Kwenye Video za Rayvanny

Kuonekana kwa Fahyma kwenye video ya Touch kunamfanya afikishe jumla ya video saba (7) alizocheza kama mhusika mkuu (video vixen) na mpenzi wake huyo.

Tofauti na warembo wengine, Fahyma ana rekodi ya kipekee zaidi nchini: Hajawahi kutokea kwenye video ya msanii mwingine yeyote yule duniani zaidi ya Rayvanny.

Orodha ya video 7 alizofanya Fahyma na Rayvanny ni pamoja na:

  • Kwetu (2016) – Wimbo uliomtambulisha Rayvanny (Fahyma alicheza nafasi ndogo).

  • Natafuta Kiki (2016)

  • Siri (2017)

  • Forever (2023)

  • Habibi (2023)

  • Mwambieni (2023)

  • Touch (2026)

Ushindani wa Rayvanny na Fahyma vs Marioo na Paula

Ingawa Rayvanny na Fahyma wana rekodi hii kubwa, si wao pekee wenye video 7 za pamoja. Rekodi hiyo pia inashikiliwa na msanii Marioo na mpenzi wake Paula ambao wamewahi kushirikiana kwenye video saba (Lonely, Tomorrow, Sing, Hakuna Matata, My Daughter, Unachekesha, na Tete).

Hata hivyo, tofauti kubwa kati ya warembo hawa wawili ni kwamba:

  1. Fahyma: Hajawahi kufanya video na msanii mwingine yeyote nje ya Rayvanny.

  2. Paula: Kabla ya kuwa na Marioo, alishawahi kutokea kwenye video ya Rayvanny (Wana Weweseka – 2021).

Video Iliyopata Mafanikio Makubwa Zaidi

Katika video zote saba za Rayvanny na Fahyma, video ya wimbo “Kwetu” (2016) ndiyo inayotawala ikiwa na zaidi ya tazamio (views) Milioni 48.5 kwenye mtandao wa YouTube. Video hii iliongozwa na Muongozaji Godfather kutokea Afrika Kusini, huku Fahyma akitokea mwishoni kabisa na kuacha alama iliyodumu hadi leo.

Licha ya changamoto na milimani na mabonde ya mahusiano, Fahyma anabaki kuwa nguzo muhimu nyuma ya mafanikio ya Rayvanny tangu akiwa WCB Wasafi hadi sasa anapomiliki lebo yake ya NLM na kushinda tuzo kubwa za kimataifa kama BET Awards, Afrimma, na Zikomo.

Fainali ya WAFCON: Cameroon vs Malawi Kutakatisha Zaidi ya Sh5.1 Bilioni Safari ya Kutimiza Ndoto Zako Inaanzia Hapa