Habari za michezo

YANGA WAENDELEA KUKISUKA UPYA KIKOSI CHAO KIMYA KIMYA…KIFAA KIPYA KUTOKA BURUNDI HIKI HAPA….

admin April 15, 2022 8:54 am

 


Wakati Msimu wa 2021/22 ukielekea ukingoni huku Young Africans ikipewa nafasi ya Kutwaa Ubingwa wa Tanzania Bara kwa mara ya kwanza baada ya miaka minne, klabu hiyo inatajwa kuanza mikakati ya kukiboresha kikosi chao kuelekea msimu ujao wa 2022/23.

Young Africans ambayo msimu huu imeonesha kuwa na kikosi imara na kipana, inatajwa kuanza mazungumzo ya kumsajili kiungo wa ushambuliaji wa raia wa Burundi , Abedi Bigirimana anayekipiga katika klab ya Kiyovu Sports ya Rwanda.

Taarifa za awali zimeeleza kuwa kwa sasa baadhi ya viongozi wa Young Africans wamepanga kusafiri kuelekea Rwanda kwa ajili ya kumfuatilia kwa ukaribu zaidi kabla hajasaini mkataba wa kuitumikia timu hiyo.

Hata hivyo hadi sasa haijaelezwa ni mchezaji gani wa kigeni atatemwa ndani ya Young Africans ili kupisha usajili wa Abedi Bigirimana ambaye anapewa nafasi kubwa ya kutua klabuni hapo.

USAJILI WA ONYANGO YANGA WAZIDI KUPINGWA…DISMAS TEN AIBUKA NA KUFUNGUKA HAYA… KUELEKEA MECHI NA WASAUZI…’TSHABALALA’ AVUNJA UKIMYA SIMBA… AIBUKA NA KAULI HII YA KIBABE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply