Habari za michezo

BAADA YA KUTINGA FAINAL YA FA…TUCHEL AWAVURUMISHIA KOMBORA LA MANENO YA KEJELI LIVERPOOL…

admin April 18, 2022 4:34 pm


Kocha mkuu wa timu ya Chelsea Thomas Tuchel amewaambia waandishi kwamba hajali kuhusu mawindo ya mataji kwa Liverpool msimu huu.

Liverpool wapo katika nafasi kubwa ya mbio za ubingwa wa EPL, pia wametinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa lakini tayari wametwaa taji la Carabao kwa kuifunga Chelsea kwenye mikwaju ya penati.

Chelsea wataumana na Liverpool katika fainali ya FA Cup mwezi Mei 14 katika uwanja wa Wembley na hii inakuwa fainali ya tatu mfululizo kwa Chelsea katika michuano hiyo na kupoteza kwa Arsenal 2020, wakapoteza kwa Leicester Cuty 2021 na sasa Liverpool.

“Sijali kuhusu mataji mengine ya Liverpool,” alisema kocha huyo wa The Blues

“Ndiyo tulipoteza Carabao Cup tulifanya kila kitu lakini bahati haikuwa kwetu kama mnavyo jua mpaka tulipokosa penati ya mwisho.

“Tutajiandaa vyema dhidi ya timu imara ulimwenguni kwa sasa, itakuwa mechi ngumu na tutajaribu kufanya maisha yawe magumu kwao.

KISA USHINDI WA JANA…MANARA AIPONGEZA NA KUINANGA SIMBA…”KULA NYAMA YA MTU KUNANOGA…”… NAMUNGO, TZ PRISONS ZANG’ARA LIGI KUU LEO….MOLINGA ATAKATA KINOMA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply