Habari za michezo

MASAU BWIRE AITAMBIA YANGA….AFUNGUKA JINSI WATAKAVYOUTUMIA UWANJA KUSHINDA MECHI HIYO…

admin April 18, 2022 4:43 pm


MASAU Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting amesema kuwa wakimalizana na Namungo leo kituo kinachofuata ni dhidi ya Yanga.

Ruvu Shooting wameomba mchezo wao dhidi ya Yanga uchezwa Uwanja wa Lake Tanganyika,Kigoma na unatarajiwa kuchezwa Mei 4,2022.

Masau Bwire amesema kuwa kila mchezo kwao ni muhimu na wanaimani ya kupata pointi tatu kutokana na uimara wa kikosi chao.

“Tuna mechi dhidi ya Namungo FC Uwanja wa Ilulu hapo tukimalizana nao tarehe 18 tunajiandaa kupambana nao hapo tutakutana na Yanga.

“Tunawapeleka kwenye uwanja ambao tumeutafakari kwa muda, (Lake Tangayika) kwa mujibu wa kanuni ya 9 kifungu kidogo cha 7 kinaturuhusu kuwapeleka uwanja mwingine na hilo inatupasa tufanye ndani ya siku 21.

Leo Apili 18, Ruvu Shooting wana mchezo wa ligi dhidi ya Namungo ambao ni wa mzunguko wa pili ikiwa ni Jumatatu ya Pasaka ambapo hata hivyo wamefungwa kwa jumla ya goli tatu kwa moja.

NAMUNGO, TZ PRISONS ZANG’ARA LIGI KUU LEO….MOLINGA ATAKATA KINOMA… SIMBA WAAPA…VIGOGO SIMBA WAO MAPEMA TU…KOCHA MOROKA AWAPA MBINU…..YANGA WAANZA TIZI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply