Habari za michezo

JEMEDARI SAID: MANARA AMELIPA PESA ILI NISIINGIE STUDIO…SIWEZI KUMKIMBIA…

admin April 28, 2022 7:59 am


Mchambuzi wa Michezo nchini Tanzania Jemedari Said amemaliza utata uliojitekeza baada ya kuibuka tetesi kuwa amemkimbia Haji Manara katika Studio za Kituo cha Radio EFM jana Jumatano (April 27).

Jemedari ametoa ufafanuzi wa jambo hilo, ambalo limechukuliwa kama sehemu ya kuendelea kwa mikwaruzano kati yake na Haji Manara ambaye mara kadhaa wamekua wakipingana katika baadhi ya hoja wanazozianika kwenye mitandao ya Kijamii ama kuzungumza kupitia vyombo vya Habari.

Baada ya kuibua kwa tetesi za kumkimbia Haji Manara Studio, Jemedari alitumia muda wake kwa kuandika kwenye ukurasa wake wa Twitter: “Naombe ieleweke, huwa SIKIMBII interview na Haji, tushafanya mara kadhaa, ila yeye ndiye alieomba kwa Viongozi wangu NISIINGIE kwenye interviews zake, sababu anazijua yeye. Mind you,this is people’s business, kama hii ya leo ni promotions ya mechi yao, wao wamelipia kama wateja.”

Haji Manara alifanyiwa mahojiano na Radio EFM leo Jumatano kwa ajili ya kuzungumzia maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Young Africans itakayokuwa mwenyeji dhidi ya Simba SC, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam Jumamosi (April 30).

BUMBULI – HATA TUKIFUNGWA NA SIMBA TUTAENDELEA KUWA NA FURAHA TU… RASMI..BAADA YA PABLO KUSHINDWA KUIPELEKA SIMBA NUSU FAINAL CAF…UONGOZI WAAFIKIANA HILI….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply