Habari za michezo

KWENYE MEI MOSI JANA…STAILI YA MAYELE YA KUTETEMA YAPIGWA MBELE YA RAIS SAMIA…WATU WAPAGAWA..

admin May 2, 2022 1:51 am


Mtindo wa ushangiliaji wa mshabuliaji Yanga, Fiston Mayele umebamba katika kilele cha maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Dunia jana yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Bendi ya Muziki ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) waliibua shangwe kwa wananchi baada ya kutumbuiza huku wakicheza aina hiyo maarufu tetema.

Vijana waliokuwa wamekaa Jukwaa la upande wa pili walianza kushangilia kabla ya mashabiki kuanza kupiga kelele za shangwe wakiwaiga.

JKT walikuwa wanaimba wao wakitikisa mabega na kupeleka kichwa mbele hali iliyowafanya wanafunzi kuinuka na kuanza kuwaiga na watu wakaanza kushangilia.

Hata hivyo juzi mchezaji huyo alishindwa kutetema baada ya timu yake kutoka suluhu ya bila kufungana walipocheza na watani zao Simba.

Kama Mayele angefunga katika mchezo dhidi ya watani huenda kelele zingekuwa za juu uwanjani hapo kutoka kwa mashabiki na wapenzi wa Yanga.

WALICHOFANYA INONGA NA MAYELE KWA MASHABIKI WA YANGA JUZI…KILA MMOJA ALIWAINUA KUSHANGILIA.. BAADA YA KUISHINDWA SIMBA JUZI….YANGA WAPAA KWA HASIRA ZOTE KWENDA KIGOMA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply