Habari za michezo

ILE ISHU YA AZIZ KI KUTUA YANGA IMEFIKIA HATUA HII AISEE…YACOUBA ATAJWA KUTIA MKONO…

admin May 6, 2022 9:57 am


UNAAMBIWA dili la Stephen Aziz Ki kujiunga na Yanga, lina mkono mkubwa wa nyota wa timu hiyo, Yacouba Songne ambaye ni rafiki yake mkubwa.

Yacouba na Aziz Ki ni marafiki wa muda mrefu ambao wote ni raia wa Burkinafaso ambapo wamewahi kucheza pamoja nchini kwao kabla ya kila mtu kwenda kusaka maisha kwingine.

Chanzo cha ndani kutoka Yanga, kimesema kuwa, timu hiyo ipo karibu kukamilisha dili la nyota huyo wa ASEC Mimosas ya Ivory Coast, huku Yacouba akiwa na msaada mkubwa wa kusimamia dili hilo kutokana na ukaribu alionao.

“Yanga wamekuwa na mazunguzmo ya muda sasa na Azizi Ki, kwa kiasi kikubwa Yacouba Songne amekuwa akihusika katika usajili huo kutokana na ukaribu wao.

“Yacouba na Aziz ni marafiki na ametumika katika kuwaunganisha viongozi wa Yanga na uongozi wa mchezaji, hivyo bado wapo katika mazungumzo.

“Yanga bado ipo katika harakati za kuhakiksha wanampata Aziz Ki ambaye anamudu vema kucheza kama winga na namba 10, mazungumzo bado yanaendelea kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa,” kilisema chanzo hicho.

Alipotafutwa  Yacouba juu ya Azizi Ki kutua Yanga, alisema: “Aziz Ki ni rafiki yangu na tulicheza wote tukiwa Burkinafaso, kuhusu kuja Yanga, kuzungumzia hilo kwa sasa ni ngumu kwa kuwa bado ni mchezaji wa ASEC, lakini kila kitu kinawezekana.”

BAADA YA KUWA NA HAKIKA HAWAPATI UBINGWA…AHMED ALLY ADAI LIGI NI DHAIFU..NA SIMBA NI DHAIFU… DEWJI AINGILIA KATI ISHU YA  MOSES PHIRI  NA ADEBAYOR KUTUA SIMBA…AAGIZA WASAJILIWE HARAKA….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply