Habari za michezo

BAADA YA KUWA NA HAKIKA HAWAPATI UBINGWA…AHMED ALLY ADAI LIGI NI DHAIFU..NA SIMBA NI DHAIFU…

admin May 6, 2022 2:52 am


Wakati mshike mshike wa Ligi Kuu Tanzania bara ukiendelea kurindima nchini, imeripotiwa kuwa kumekuwa na udhaifu mkubwa wa kiushindani hali inayohatarisha ubora uliokuwepo kwa misimu kadhaa iliyopita.

Hayo yanafuatia Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally kuandika kwenye mitandao yake ya kijamii akihoji kuwa iweje hadi sasa takribani timu 14 zigombanie kutokushuka daraja huku ikiwa tayari raundi 22 zimeshachezwa.

Katika ukurasa wake wa Instagram, Ahmed Ally ameandika ”Kati ya timu 16, timu 14 zinaweza kushuka daraja, hii sio aina ya Ligi tunayoihitaji haiwezekani timu nyingi zigombanie kushindwa.

Ligi yenye ushindani ni ile ambayo timu nyingi zinagombania ubingwa, lakini msimu huu timu nyingi dhaifu, tupo raundi ya 22 lakini ni timu tatu tu zimefikisha alama 30+.

Msimu uliopita hadi kufikia raundi ya 22 japo timu zilikuwa nyingi lakini timu 7 zilikua na alama zaidi ya 30,hii ni hatari kwa sababu bingwa anaweza kupatikana kwa kufunga wadhaifu wengi.

Najua utauliza kwanini na wewe usiwafunge hao dhaifu wengi ili uwe bingwa, ukweli ni kwamba katika hizo mechi zetu dhidi ya timu dhaifu nasi tulifanya udhaifu.”Ahmed Ally Afisa Habari wa Simba.

KUELEKEA MECHI NA AZAM FC…HITIMANA NA KMC YAKE WAOMBA MUNGU AWAKUMBUKE HATA NA SARE TU… ILE ISHU YA AZIZ KI KUTUA YANGA IMEFIKIA HATUA HII AISEE…YACOUBA ATAJWA KUTIA MKONO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply