Habari za michezo

KUELEKEA MECHI YA LEO DHIDI YA RUVU…MATOLA AVUNJA UKIMYA SIMBA…AFUNGUKA HALI ILIVYO NDANI…

admin May 8, 2022 8:00 am


Kocha Msaidizi Seleman Matola, amesema kikosi kipo tayari kwa mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi Ruvu Shooting utakaopigwa Uwanja kwa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Matola amesema baada ya kurudi kutoka mkoani Lindi katika mchezo dhidi ya Namungo kikosi kiliingia kambini moja kwa moja tayari kwa mtanange huo.

Matola amesema hatujapata ushindi katika michezo mitatu iliyopata lakini jambo hilo halijashusha morali yetu na tumejipanga kuhakikisha tunapata ushindi.

“Tunajua mchezo utakuwa mgumu, Ruvu ni timu nzuri na ipo kwenye nafasi mbaya katika msimamo hivyo wanahitaji ushindi ili kujinasua lakini tupo tayari kuwakabili.

“Kikosi kipo kwenye hali nzuri wachezaji wote wapo tayari isipokuwa Hassan Dilunga na Sadio Kanoute ambao ni majeruhi,” amesema Matola.

BAADA YA MANARA KUMSHUKIA ‘JUMLA JUMLA’…AHMED ALLY AOMBA MSAMAHA KAULI YA UDHAIFU WA VILABU…. GEITA GOLD YAWASHA TAA MCHANA….WAIKUNG’UTA KAGERA ‘CHA UCHUNGU’…MPOLE NA MAYELE SAWA TU…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply