Habari za michezo

A-Z JINSI YANGA WALIVYOINYONGA SIMBA NDANI YA UWANJA …WALITANGULIZA ‘MASHINE’ MBILI MBELE…TABU IKO PALEPALE…

admin May 29, 2022 2:22 am


KLABU ya Yanga imefanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam baada ya kuifunga klabu ya Simba kwa jumla ya bao 1-0 bao lililofungwa na Feisal Salum kipindi cha kwanza cha mchezo.

Mchezo ulikuwa na kasi huku timu zote zikifanikiwa kutengeneza nafasi za mabao lakini umakini ulikuwa mdogo kwa washambuliaji wa pande zote mbili ikiongozwa na Yanga ambayo ilicheza na washambuliaji wawili Fiston Mayele pamoja na Heritier Makambo.

Mchezo ulishuhudia majeruhi wawili Kibwana Shomari pamoja na Kibu Denis ambao walipata majeraha ya kichwa baada ya kugongana kwenye mpira wa juu.

Nusu fainali ya pili inatarajiwa kuchezwa leo kati ya Azam na Coastal Union ambayo mshindi baina yao ataungana na klabu ya Yanga katika kucheza fainali ya kombe hilo la Shirikisho mkoani Arusha.

NI MADRID TENAAH….WAENDELEZA UBABE WA LIGI YA MABINGWA ULAYA…LIVERPOOL NI SAWA NA SIMBA SC WALIOCHANGAMKA…. KUELEKEA MECHI YAO NA COASTL UNION LEO…KOCHA MSOMALI WA AZAM APANGA KUINGIA NA GIA ZA SIMBA….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply