Azam FC

AZAM FC WAMSHUSHIA LAWAMA MWAMUZI WA JANA…WADAI IMETOSHA…WAHOJI KWA NINI KILA SIKU WAO TU..?

admin May 19, 2022 9:20 am


Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino Azam FC Thabit Zakaria ‘Zakazakazi’ amelitaka Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ kupitia kamati ya Waamuzi, kumfikiria Mwamuzi mwingine tofauti na Heri Sasii ambaye anadaiwa kuchezesha michezo muhimu na mikubwa kwa klabu hiyo.

‘Zakazakazi’ ametoa ombo hilo TFF, baada ya Mwamuzi huyo kuchezesha mchezo wa jana Jumatano (MEi 18), dhidi ya Simba SC kwenye Uwanja wa Azam Complex-Chamazi jijini Dar es salaam na timu hizo kuambulia matokeo ya 1-1.

‘Zakazakazi’ amesema Mwamuzi huyo kwa msimu huu amechezesha mchezo wao dhidi ya Young Africans kisha alipewa nafasi hiyo katika mchezo dhidi ya Simba SC na jana amerejea tena Dimbani kuchezesha mchezo dhidi Mabingwa hao wa Tanzania Bara.

“Tumechoka na Heri Sasii, kwani hakuna waamuzi wengine ? Tunaiomba bodi ya ligi isitupangie tena mwamuzi Heri Sassi”,

“Kwa nini michezo yetu yote dhidi ya Simba anachezesha Heri Sassii, mechi ya Round ya kwanza alichezesha Sassii, mechi yetu dhidi ya Yanga alichezesha Herri Sassi, mechi ya Round ya pili dhidi ya Simba kachezesha Sassiii,, kwani hakuna waamuzi wengine ?!” amehoji ‘Zakazakazi’

BAADA YA SIMBA KUPATA SARE JANA…AHMED ALLY AIBUKA NA KULIA NA HILI…”YAMETUACHA NA HUZUNI..WANAMASONONEKO”… KAMERA ZA AZAM TV ZILIVYOMNASA NABI AKIWA ANAIPIGA SIMBA CHABO CHAMAZI JANA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply