Kagera Sugar Said Ndemla
Michezo Bongo

Kagera Sugar Yakaribia Kumsajili Said Ndemla Wa JKT Tanzania

Vardo August 2, 2026 10:24 am

Uongozi wa klabu ya Kagera Sugar umeingia kwa kasi kwenye soko la usajili mara tu baada ya kufanikiwa kupanda tena kucheza Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2026/2027.

Mabosi wa klabu hiyo maarufu kama ‘Wanankurukumbi’ wapo kwenye hatua za mwisho kabisa kumpata kiungo mkabaji na mzoefu wa zamani wa JKT Tanzania na Simba SC, Said Ndemla.

Ndemla, ambaye ni stadi wa kucheza nafasi ya kiungo cha kati na anayejulikana kwa pasi zake za mwisho pamoja na mashuti ya mbali, anadaiwa kufikia makubaliano ya awali ya kujiunga na kikosi hicho.

Nyota huyo alijiunga na JKT Tanzania mnamo Julai 24, 2023 akitokea Fountain Gate, na sasa ameweka wazi kuwa mkataba wake na Maafande hao umehitimishwa—jambo lililowapa mwanya Kagera Sugar kuongeza kasi ya kuwania saini yake licha ya klabu nyingine kadhaa kuonyesha nia.

Kauli ya Uongozi wa Kagera Sugar

Akizungumzia Mipango ya usajili ndani ya klabu hiyo, Meneja wa Kagera Sugar, Bernard Samson Sikira, amethibitisha kuwa mchakato wa kusuka kikosi kipya umeanza ramsi:

“Suala zima la usajili limeanza tayari. Japo utambulisho rasmi wa nyota wapya watakaokitumikia kikosi chetu kwa msimu ujao wa 2026/2027 utaanza kufanyika siku chache zijazo.”

Wachezaji Wengine Wapya Kujiunga na Kagera Sugar

Mbali na Said Ndemla, Kagera Sugar ipo kwenye mazungumzo ya mwisho kumsajili pamoja na wachezaji wengine wapya wanaotajiwa kuimarisha kikosi hicho:

  • Dickson Mhilu (Beki wa kulia – Dodoma Jiji)

  • Daudi Milandu (Kiungo – Dodoma Jiji)

  • Boniface Onyango (Beki wa kushoto/kati – Kakamega Homeboyz, Kenya)

  • Collins Maina (Mshambuliaji – Fortune Sacco FC, Kenya)

  • Naku James (Mshambuliaji – Polisi Tanzania)

Usajili huu unaonyesha dhamira ya dhati ya Kagera Sugar kufanya vizuri na kujihakikishia nafasi ya ushindani wa juu kwenye Ligi Kuu Bara msimu ujao.

Dodoma Jiji Yaingia Vitani Kumnasa Mussa Mbisa wa Tanzania Prisons!